IQNA

Rais Mpya wa Mauritania ni Hafidh wa Qur'ani Tukufu

17:32 - August 04, 2019
Habari ID: 3472069
TEHRAN (IQNA)- Rais mpya wa Mauritania, Mohammad Ould Ghazouani, amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Kwa mujibu wa taarifa, Ghazouani ambaye alichukua hatamu za urais Agosti Mosi alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani akiwa katika shule ya msingi.
Ghazouani alizaliwa Boumdeid, eneo la Assaba kusini mwa Mauritania, mwaka 1956 na ametoka katika familia maarufu ya Kisufi (twariqa) nchini humo. Ghazouani ni mwana wa kiongozi wa kabila la Ideiboussat.
Mwezi Juni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Mauritania ilitangaza rasmi kuwa, waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi hiyo, Mohammad Ould Ghazouani ndiye mshindi katika uchaguzi wa rais. Ghazouani ni mtu wa karibu sana na rais aliyeondoka wa nchi hiyo, Mohammed Ould Abdel Aziz.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Mauritania iiliema kuwa, Ghazouani ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 52.01 ya kura.
Mkuu wa tume hiyo ya uchaguzi, Ould Bilal, amewaambia waandishi wa habari kwamba uchaguzi huo ni ushindi kwa taifa la Mauritania na umetia nguvu misingi ya kidemokrasia nchini humo.

3832219

Kishikizo: iqna mauritania
captcha