IQNA

Katika Siku ya Kimataifa ya Msikiti

Hamas yakosoa nchi za Kiarabu kwa kupuuza kadhia ya Msikiti wa Al Aqsa, yapongeza msimamo wa Iran

18:47 - August 21, 2019
Habari ID: 3472094
TEHRAN (IQNA)- Mjumbe wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) mjini Tehran amezikosoa nchi za Kiarabu kwa kuzembea kuhusu kadhia ya kuukomboa Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) ambao unakaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Khaled al-Qaddumi, mjumbe wa Hamas mjini Tehran ameyasema hayo akiwa  katika Kongamano la 17 la Siku ya Kimataifa ya Msikiti na kuongeza kuwa: "Inasikitisha kuona nchi za Kiarabu hazichukui hatua zozotoe za maana za kuukomboa Msikiti wa Al Aqsa unaokaliwa kwa mabavu."

Al-Qaddumi ameongeza kuwa: "Hatua za kijuba za rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Palestina na Quds Tukufu ni natija ya kukaa kimya nchi za Kiarabu."

Mjumbe wa Hamas mjini Tehran aidha ameishukuru kwa dhati Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono kadhia ya ukombozi wa Msikiti wa Al Aqsa na Palestina na kuongeza kuwa: "Nafasi athirifu ya Iran katika kadhia ya Palestina haiwezi kuliganishwa hata kidogo na ile ya nchi zingine duniani."

Khaled al-Qaddumi ameashiria kumbukumbu ya jinai ya Wazayuni kuuteketeza moto Msikiti wa Al Aqsa na kusema: "Msikiti wa Al Aqsa na kadhia ya Palestina ni nukta za pamoja za Waislamu wote duniani."

Ikumbukwe kuwa tarehe 21 mwezi Agosti ni maadhimisho ya kuchomwa moto na Wazayuni msikiti wa al Aqsa miaka 50 iliyopita yaani mwaka 1969. Kufuatia pendekezo la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu, OIC, imeitangaza siku hii kuwa Siku ya Kimataifa ya Misikiti.

Kuchomwa moto msikiti wa Al Aqsa ambacho ni kibla cha kwanza cha Waislamu na moja ya maeneo matukufu ya kidini ya dini za mbinguni kulikojiri Agosti 21 mwaka 1969, ni uthibitisho mwingine wa jinai za utawala wa Kizayuni na ni doa jeusi kwa maghasibu wanaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu ambalo halitafutika milele.   

Tukio hilo la kuuchoma moto msikiti mtakatifu wa al Aqsa lilikabiliwa na hasira na ghadhabu za Waislamu duniani kote. Aidha   utawala wa Kizayuni uliilinasibisha tukio hilo na mtalii mmoja Myahudi mwenye misimamo ya kufurutu ada raia wa Australia kwa jina la Denis Michael; ambapo mtalii huyo alifikishwa mahakamani na kuhukumiwa na kisha akaachiwa huru kwa madai kwamba ni mgonjwa wa akili. 

2505372

captcha