IQNA

Ismail Hania amshukuru Kiongozi Muadhamu kwa mazungumzo na ujumbe wa Hamas

20:08 - September 02, 2019
Habari ID: 3472110
TEHRAN (IQNA) - Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amemuandikia barua Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kushukuru yale aliyoyazungumza katika mkutano wake na ujumbe wa harakati hiyo uliofanya ziara hapa mjini Tehran hivi karibuni .

Katika barua hiyo, Ismail Hania ameshukuru na kupongeza uungaji mkono wa wazi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa muqawama wa Palestina pale alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Hamas uliokuwepo ziarani mjini Tehran. Ayatullah Khamenei alisema Iran iko tayari kuipa Hamas suhula zozote zinazohitajika kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake.

Katika barua hiyo, Hania amemhutubu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akisema: Namshukuru Mwenyezi Mkubwa kwa uwepo wenu wa thamani kwa ajili yetu; na nimamuomba awaruzuku neema zake, awaepushe na mabalaa na njama na shari za maadui. Katika barua hiyo, Hania aidha amemuomba Mwenyezi Mungu ajalie kheri na baraka, atimize maombi yote ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi; aujalie kheri Umma wa Kiislamu upate ushindi, uwe na nguvu, usalama, maadui waangamizwe na Palestina ikombolewe pamoja na Quds Tukufu.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas aidha ameshukuru namna Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliovyoukaribisha ujumbe wa Hamas hapa Tehran. Saleh al Aruri Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas na ujumbe aliofuatana nao tarehe 22 mwezi Julai mwaka huu walikutana na kufanya mazungumzo hapa Tehran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. 

Katika mkutano huo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya alisisitiza kuwa, kadhia ya Palestina ndiyo kadhia nambari moja na ndilo suala muhimu zaidi kwa Ulimwengu wa Kiislamu.

Aidha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekusifu kusimama imara na muqawama wa kustaajabisha wa wananchi wa Palestina pamoja na makundi ya muqawama likiwemo la Hamas na akasisitiza kwa kusema: Ushindi haupatikani bila muqawama na mapambano, na kwa mujibu wa ahadi isiyokhalifu ya Allah, sisi tunaitakidi kuwa, hatima ya maudhui ya Palestina bila shaka itakuwa kwa manufaa ya watu wa Palestina na Ulimwengu wa Kiislamu.

3473586

captcha