IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Vita dhidi ya Iran vitapelekea utawala wa Israel ufutwe katika uso wa dunia

21:20 - September 10, 2019
Habari ID: 3472123
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema mbele ya mjumuiko mkubwa wa Waislamu katika maombolezo ya Siku ya Ashura ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein AS kwamba, vita vyovyote vile dhidi ya Iran vitakuwa na maana ya kuangamizwa na kufutwa katika uso wa dunia, dola pandikizi la Israel.

Akizungumza kwa njia ya moja kwa moja kupitia Televisheni ya Al Manar ya Lebanon leo Jumanne adhuhuri , Sayyid Hassan Nasrallah amesisitiza kwa mara nyingine kwamba, kambi ya muqawama itaendelea kuwa pamoja na wananchi wa Palestina na Yemen. Amesema, kile kinachoshuhudiwa hivi sasa kusini mwa Yemen ni ushahidi wa wazi kwamba wavamizi wa nchi hiyo yaani Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) wanauangalia kwa jicho la tamaa utajiri wa Yemen lakini matokeo ya vita walivyovianzisha dhidi ya nchi hiyo si kitu kingine ghairi ya kushindwa na kupata aibu ya kihistoria wavamizi hao.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na Syria ni vya kidhulma na kusisitiza kwamba, baada ya kushindwa Israel katika vita vyake huko Paletina na Lebanon na kuendelea kushindwa magenge ya kigaidi na ukufurishaji katika nchi za Lebanon, Syria na Iraq, hivi sasa serikali ya Marekani haikuona njia nyingine isipokuwa kukimbilia kwenye vikwazo vya kifedha. 

Amesema, Hizbullah ya Lebanon itaendelea kuheshimu azimio nambari 1701 la Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa, muqawama (Hizbullah) na asasi nyingine zote za Lebanon zina haki ya kujihami na iwapo utawala wa Israel utaivamia tena Lebanon, basi muqawama wa nchi hiyo uko tayari kutoa majibu makali na kwa muda unaofaa, na hakutakuwa na mstari wowote mwekundu katika kukabiliana na chokochoko za utawala huo wa Kizayuni.

3841311

captcha