Taarifa zimesema wakuu wa mji wa Helsiniki wanakataa kuidhinisha ujenzi wa msikiti huo kwa sababu unafadhiliwa na utawala wa Bahrain unaoongozwa na ukoo wa Aal Khalifa.
Vyombo vya habari nchini Finland vimesema hali ya kisiasa nchini Bahrain na hatua ya utawala wa Aal Khalifa kukandamiza maandamano ya amani nchini humo ni kati ya sababu zilizopelekea kutopata kibali cha ujenzi msikiti huo.
Wasimamizi wa mradi huo wanasema msikiti huo ulikuwa unatazamiwa kuwa na nafasi za watu 2100 ikiwa ni pamoja na suhula za afya na michezo.
Tangu mwezi Februari 2011 hadi sasa, Bahrain inaendelea kushuhudia wimbi la malalamiko ya wananchi wanaotaka mageuzi ya kisiasa, kuweko utawala wa sheria, kufanyika uchaguzi huru na wa kidemokrasia na kuondolewa ubaguzi na upendeleo wa kimadhehebu na kikaumu nchini humo.
3464729