IQNA

Wiki ya Qur'ani Tukufu inafanyika Algeria

11:02 - December 21, 2017
Habari ID: 3471319
TEHRAN (IQNA)-Duru ya 19 ya "Wiki ya Kitaifa ya Qur'ani" ya Algeria imeanza kuadhimishwa Disemba 19 katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Shughuli hiyo imeandaliwa na Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini nchini Algeria chini ya kaulimbiu ya 'Malezi ya Kimaanawi katika Qur'ani."

Sherehe hizo  za uzinduzi wa 'Wiki ya Kitaifa ya Qur'ani" zilihudhuriwa na  wageni 600 wakiwemo wanazuoni wa Kiislamu, wanasiasa, mabalozi na wahadhiri wa vyuo vikuu  ambao walihudhuria sherehe iliyofanyika katika mji mkuu Algiers.

Akihutubu katika sherehe hizi, Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kidini Algeria Muhammad Issa alisisitiza ulazima wa kustawisha thamani za Qur'ani katika jamii.

Aidha alitoa wito kwa wanaharakati katika sekta mbali mbali kujitahidi kuinua viwango vya umaanawi.

Katika wiki ya Qur'ani nchini Algeria hufanyika hafla mbali mbali hasa mihadahra ya kidini kuhusu nafasi ya taasisi za kidini katika maelzi ya Kiislamu na pia vikao vya usomaji Qur'ani.

3464722

captcha