IQNA

Mashindano makubwa zaidi ya Qur'ani duniani mubashara katika televisheni kufanyika Iran

11:13 - May 05, 2018
Habari ID: 3471494
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Qur’ani ya kimataifa yanayofanyika kwa njia ya moja kwa moja kupitia Televisheni ya Al Kauthar ya Iran yamepangwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani siku chache zijazo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mashindano ya 11 ya Kimataifa ya Qur’ani ya إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا , "Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu"  yataanza katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.  Katika mashindano hayo ya qiraa au kusoma Qur’ani yanyaofanyika kwa mwaka wa 11 sasa, washiriki kutoka kila kona ya dunia watashiriki moja kwa moja (live au mubashara) kwa njia ya simu. Katika mashindano ya mwaka huu mbali na kupiga simu, pia washiriki wanaweza kushiriki kwa njia ya taswira kupitia mtandao wa Skype. Halikadhalika mwaka huu washiriki wataweza kutumia njia ya intaneti kuona pointi walizopata wakati mashindano yakiendelea.

Majaji wa mashindano yam waka huu ni kutoka nchi kadhaa za Kiislamu kama vile Misri, Syria, Iraq na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kwa mujibu wa waandalizi, katika kila usiku wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutakuwa na washiriki watano kutoka nchi tano na katika awamu ya kwanza ya mashindano hayo, wasomaji au maqarii 25 bora watateuliwa kuingia nusu fainali na hatimaye watano watachuana katika fainali. Mashindano hayo, ambayo yametajwa kuwa makubwa zaidi ya aina yake duniani, yatakuwa yanarushwa hewani kuanzia saa tano unusu usiku(23:30) kwa wakati wa Tehran au saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki kupitia Televisheni ya Kimataifa ya Al Kauthar na fainali zitafanyika katika siku ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.  Kwa maelezo zaidi kuhusu mashindano hayo na namna ya kujisajili, bonyeza hapa.

3711388/

captcha