IQNA

Waliohifadhi Qura'ni waenziwa nchini Bulgaria

14:26 - August 30, 2019
Habari ID: 3472106
TEHRAN (IQNA) – Vijana kadhaa waliohifadhi Qur'ani Tukufu nchini Bulgaria wameenziwa na kutunukiwa zawadi.

Kwa mujibu wa taarifa sherehe hiyo, iliyofadhiliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Qur'ani na Sunna, imefanyika katika mji wa Madan ambao uko katika mkoani wa Smolyan, kusini mwa nchi hiyo ya bara Ulaya.

Waliotunukiwa zawaid ni wale waliohitimu katika kozi maalumu ya kuhifadhi Qur'ani katika Taasisi ya Abu Ayub Ansari.

Waliozugumza katika sherehe hiyo wameashiria fadhila za kuhifadhi Qur'ani huku wakitoa wito wa kuwepo vikao kama hivyo ili kuwahimiza vijana kunufaika na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

Aidha waliwahimiza waliohifadhi Qur'ani kutekeleza mafundisho ya kitabu hicho kitukufu katika maisha yao.

Bulgaria ni nchi iliyo kusini mashariki mwa Ulaya na Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia 15 ya watu wote nchini humo.

3838350

captcha