IQNA

Rais Hassan Rouhani

Iran itachukua hatua ya tatu ya kupunguza uwajibikaji katika JCPOA

11:54 - September 05, 2019
Habari ID: 3472115
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameatangaza kuwa, awamu ya tatu ya Iran kupunguza uwajibikaji wake katika makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) itaanza kutekelezwa Ijumaa.

Rais Rouhani amesema hayo Jumatano usiku mjini Tehran mwishoni mwa kikao cha wakuu wa mihimili mikuu mitatu ya dola Iran na kusisitiza kwamba, Ijumaa ya kesho ya Septemba 6 ndio siku ambayo Iran itaanza kutekeleza awamu ya tatu ya kupunguza uwajibikaji wake katika JCPOA.

Rais Rouhanii amesema, Shirika la Atomiki ya Iran kuanzia kesho Ijumaa inapaswa kuweka kando ahadi na uwajibikaji wake wote katika makubaliano ya nyuklia na kupanua utafiti na ustawi katika aina za mashinapewa mpya na kufanya urutubishaji madini ya Urani kwa kasi na kwa kadiri ya mahitaji.

Rais wa Iran amefafanua kuwa, pamoja na kuchukua hatua ya tatu, Tehran itatoa muhula mwengine wa miezi miwili kwa pande shiriki katika JCPOA; na endapo utafikiwa mwafaka, bado kuna njia ya mantiki, mazungumzo na kufikiwa makubaliano baina ya pande mbili.

Rais Rouhani amesema, subira ya kistratejia na hatua ya Iran ya kukabiliana na uamuzi wa Marekani wa kujitoa katika JCPOA vimefanyika kwa umakini kamili na akasisitiza kwamba: Hatua ya tatu ya kupunguza utekelezaji majukumu ya Iran ina umuhimu mkubwa mno na ndio hatua muhimu zaidi itakayochukuliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ameongeza kuwa, kwa agizo na amri itakayotolewa, Shirika la Nishati ya Atomiki litaweza kufikia malengo yake kwa kasi kubwa mno.

Rais wa Iran amefafanua kuwa, pamoja na kuchukua hatua ya tatu, Tehran itatoa muhula mwengine wa miezi miwili kwa pande shiriki katika JCPOA; na endapo utafikiwa mwafaka, ingaliko njia ya mantiki, mazungumzo na kufikiwa makubaliano baina ya pande mbili.

Dakta Rouhani aidha amewataja viongozi wenye mitazamo ya kufurutu mpaka katika serikali ya Marekani, utawala wa ubaguzi wa rangi wa Kizayuni na baadhi ya viongozi wenye fikra mgando katika eneo kuwa ni magenge matatu ambayo hayataki kuona uhusiano sahihi na wa kiadilifu unakuwepo baina ya Iran na Marekani; na akabainisha kuwa, kudhibitiwa Ikulu ya White House na magenge hayo matatu ndio sababu ya kujitoa Marekani katika JCPOA.

Tarehe 8 Mei mwaka huu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilisitisha utekelezaji wa baadhi ya majkumu yake katika makubaliano ya nyuklia kulingana na kifungu cha 26 na 36 vya makubaliano hayo. Mnamo tarehe 7 Julai, Iran ilianzisha pia mchakato wa kuvuka kiwango cha asilimia 3.67 cha urutubishaji madini ya urani katika shughuli zake za nyuklia.

Halikadhalika Tehran imetangaza kwamba, endapo upande wa Ulaya utaendelea kuzembea kutekeleza majukumu yake, ifikapo tarehe 6 Septemba itaanza kutekeleza awamu ya tatu ya kupunguza uwajibikaji wake katika JCPOA.../

Halikadhalika Tehran imetangaza kwamba, endapo upande wa Ulaya utaendelea kuzembea kutekeleza majukumu yake, ifikapo tarehe 6 Septemba itaanza kutekeleza awamu ya tatu ya kupunguza uwajibikaji wake katika JCPOA.

3840222/

captcha