IQNA

Muungano wa Marekani umeua watoto 920 nchini Syria

15:45 - September 24, 2019
Habari ID: 3472146
TEHRAN (IQNA) – Mtandao wa Haki za Binadamu Syria umesema hadi sasa muungano wa kijeshi unaaongozwa na Marekani umeua raia 3,000 Wasyria, wakiwemo watoto 924.

Ripoti hiyo iliyotangazwa Jumatatu kwa munasaba wa mwaka wa tano wa muungano wa kijeshi unaaongozwa na Marekani kuingia vitani Syria imebaini kuwa, wanajeshi wa muungnao huo wameshindwa kuzingatia sheria za kimataifa katika mashambulizi yao mbali na kuwasababishia watu wa Syria hasara kubwa.

Ripoti hiyo ya kurasa tisa imesema kuungano wa kijeshi unaaongozwa na Marekani wenyewe umekiri kuua raia 1,313 nchini Syria na Iraq.

Magaidi wanaopata himaya ya kigeni walianzisha hujuma dhidi ya Syria mwezi Machi 2011 na hivi sasa wametimuliwa kutoka karibu maeneo yote ya nchi hiyo.  Serikali ya Syria inasema muungano huo wa kijeshi naoongozwa na Mareknai ambao uliingia vitani nchini humo kwa kisingizio cha kupambna na magaidi, ndio ambao umekuwa ukiwaunga mkono magaidi wakufurishaji nchini humo. Magaidi nchini Syria wameangamziwa kutokana na msaada wa kijeshi kutoka Russia na Iran pamoja na wapiganaji wa Hizbullah. Serikali ya Syria iliomba rasmi msaada wa kijeshi kutoka Syria na Iran ili kukabiliana na magaidi.

3844481

captcha