IQNA

Muuza mihadarati wa zamani ahifadhi Qur'ani kikamilifu

10:41 - October 08, 2019
Habari ID: 3472162
TEHRAN (IQNA) - Muuza mihadarati wa zamani nchini Uturuki ambaye hadi sasa ametumikia kifungo cha mwaka moja na nusu gerezani amewafnaikiw akuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Abdul Qader Gilani anasema amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu katika kipindi cha miezi 15. Hivi sasa anawasaidia wafungwa wenzake katika Gereza ya Konya kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

"Wakati nilipohukumiwa kifungo cha miezi 18 gerezani, nilifahamu kuwa kuna nukta chanya katika hujumu hiyo," amesema.

"Kwa sasa, nimeamua kuwa Hafidh wa Qur'ani Tukufu. Kabla ya kuwa Hafidh sikuwa nadhani kuwa naweza kupata mafanikio hayo."

Aidha amewapongeza wakuu wa gereza kwa musaidia katika njia yake ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

3469590

 

captcha