IQNA

Mufti wa Misri: Uislamu unataka ustahamilivu na kuishi pamoja kwa amani

10:03 - November 18, 2019
Habari ID: 3472219
TEHRAN (IQNA) – Mufti Shawqi Allaam amesema Uislamu ni dini ya ustahamilivu na rehema na inataka watu waishi pamoja kwa amani na wawe na mazungumzo baina yao.

Katika taarifa kwa munasaba wa Siku ya Kimataifa ya Ustahamilivu iliyoadhimishwa Novemba 16, Sheikh Allam amesema Uislamu unaheshimu uwepo wa watu wa kaumu, rangi na makabila mbali mbali kwani hilo linaashiria uwezo na hekima ya Mwenyezi Mungu.

Amesema kustahamiliana wafuasi wa dini mbali mbali, kuishi pamoja kwa amani na kuwepo mazungumzo baina ya dini mbali mbali kunapaswa kuwa msingi wa maelewano na kupunguza malumbani duniani.

Aidha amehimiza kuwepo mazungumzo baina ya viongozi wa dini mbali mbali ili kuwepo hali ya kustahamiliana baina ya wafuasi wa dini mbali mbali.

3857581

captcha