IQNA

Watu milioni moja watembelea Bustani ya Qur'ani Dubai

11:44 - November 22, 2019
Habari ID: 3472226
TEHRAN (IQNA)- Manispaa ya Mji wa Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imetangaza kuwa watu milioni moja wameitembelea Bustani ya Qurani tangu ifunguliwe mjini humo mwezi Machi mwaka huu.

Dawood al Hajri, Mkurugenzi Mkuu wa Manispaa ya Dubai amesema bustani hiyo ilifunguliwa sambamba na Mwaka wa Ustahamilivu ili kuleta maeleano baina ya wafuasi wa tamaduni na dini mbali mbali sambamba na kuweka wazi misingi ya ustahamilivu katika Uislamu na jamii ya UAE. Lengo kuu la kuanzishwa bustani hiyo aidha limetajwa kuwa kuonyesha mafanikio ya Uislamu katika uga wa ekolojia ya mimea.

Bustani hiyo imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekari 60 na mimea yote iliyoko hapo imetajwa katika Qur'ani Tukufu. Aidha bustani hiyo ina vivutio vingine kama vile maeneo ya watoto kucheza, Kona ya Umrah, jukwaa la wazi la tamthilia, na maeneo yanayoonyesha miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu.

Manispaa ya Dubai imetangaza kuwa hakuna malipo yoyote kwa anayetaka kutembelea bustani hiyo isipokuwa tu kwa wale wanaotaka kutembelea Pango la Miujiza na Nyumba ya Kioo katika Bustani hiyo.

3469904

Kishikizo: iqna qurani bustani dubai
captcha