IQNA

Nakala ya kale zaidi ya Qur'ani China yawekwa katika maonyesho

15:17 - December 01, 2019
Habari ID: 3472245
TEHRAN (IQNA) – Nakala ya kale zaidi ya Qur'ani Tukufu nchini China imewekwa katika maonyesho ya umma kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Qinghai, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Inakadiriwa kuwa nakala hiyo iliandikwa miaka 1,000-1,300 iliyopita na ni kati ya nakala za kale zaidi za Qur'ani Tukufu duniani.

Nakala hiyo ina kurasa 867 na Juzuu zote 30 na ina uzito wa kilo 12,79 huku ikiwa na jildi ya ngozi ya kifaru na nakshi za kuvutia.

Mwaka 2009, nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu iliwekwa katika Orodha ya Kitaifa ya Vitabu Nadra vya Kale.

Hivi sasa nakala hiyo ya Qur'ani imewekwa katika sanduku maalumu la kioo ambapo viwango vya oxigeni, nyuzi joto na unyevunyevu vinadhibitiwa.

Kwa mujibu wa maelezo, nakala hiyo ya Qurani ililetwa katika eneo hilo na Waislamu wa  kaumu ya Salar ambapo awali walikuwa wakiishi Asia ya Kati kabla ya kuhamia Kaunti ya Salar, eneo la Xunhua katika mkoa wa Qinghai katika karne ya 13 Miladia. Hivi sasa nakala hiyo ya kale ya Qur'ani imehifadhiwa katika Msikiti wa Jiezi na inakadiriwa kuwa kila siku watu 6,000 hufika msikitini hapo kuitazama.

3470002

captcha