IQNA

Wanawake Uzbekistan washiriki katika mashindano ya Qur'ani

15:45 - December 01, 2019
Habari ID: 3472247
TEHRAN (IQNA) – Wanawake nchini Uzbekistan wameshiriki katika mashindano ya Qur'ani ambaye yamefanyika hivi karibuni katika mji mkuu, Tashkent.

Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo yaliyopewa jina la 'Nyoyo Zetu, Makao ya Qur'ani' yamewashirikisha wanawake ambao ni wanachama wa Taasisi ya Kiislamu ya Tashkent.

Jopo la majaji katika mashindano hayo lilijumuisha wanazuoni wa ngazi za juu wa Qur'ani nchini humo wakiwemo Jahangir Nematov, Adhamjan Qari Rashidov, na Valikhan Qari Azimbayov.

Washindi watatu wa kwanza katika kila kategoria walitunukiwa zawadi.  Uzbekistan ni nchi ya Asia ya Kati. Imepakana na Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan.

Uzbekistan ni nchi yenye historia ndefu. Miji yake kama vile Ferghana, Tashkent, Bukhara, Khwarezm na Samarkand zilikuwa vitovu vya utamaduni wa binadamu tangu milenia ya 2 Kabla ya Miladia (BC). Nchi hiyo ni mashuhuri kwa misikiti yake na asilimia 96 ya watu wa nchi hiyo ni Waislamu.

3860454

captcha