IQNA

Wasomi 40 kutayarisha tarjumi ya Qur'ani kwa Kirussia

14:10 - December 02, 2019
Habari ID: 3472249
TEHRAN (IQNA) – Timu ya watu 40 wakiwemo wakalimani na wanazuoni wa Uislamu wanatazamiwa kuanza kuandika tarjumi mpya ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kirussia.

Wasomi 40 kutayarisha tarjumi ya Qur'ani kwa KirussiaHayo yamesemwa na Sheikh Kamil Samigullin pembizoni mwa mkutano wa ‘Kundi la Maono ya Kistratijia ya Russia na Ulimwengu wa Kiislamu’ ambao unafanyika katika mji wa Ufa katika Jamhuri ya Bashkorostan nchini Russia.

Alisema  ili kuandika tarjumi sahihi ya Qur'ani kuna haja ya kufahamu kikamilifu lugha za Kiarabu na Kirussia na pia kuelewa  masuala ya kidini na kihistoria pamoja na lahaja mbali mbali.

Amsema kwa kuzingatia kuwa ni vigumu kwa mtu moja kuwa na ustadi wa nukta hizo zote, wamefikia natija kuwa jopo la watarjumi na wanazuoni wanaweza kutayarisha tartjumi bora zaidi ya Qur'ani kwa lugha ya Kirussia. Sheikh Samigullina amesema kazi ya jopo hilo inatazamiwa kuchukua muda wa miaka 7 kabla yakukamilika.

Hivi karibuni Mwanamke wa Russia aliyesilimu na kisha kutarjumi Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kirussia alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Russia, Bi. Valeria Porokhova alifariki Jumtatu. Tarjuma yake ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kirussia imetajwa kuwa miongoni mwa bora zaidi.

3860971

captcha