IQNA

Kitivo cha Qur'ani chafunguliwa katika Chuo Kikuu cha Al Qasimia Sharjah, UAE

11:40 - December 14, 2019
1
Habari ID: 3472277
TEHRAN (IQNA) – Kitivo cha Qur'ani Tukufu kimefunguliwa katika Chuo Kikuu cha Al Qasimia huko Sharjah katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Sherehe za ufunguzi zimehudhuriwa na Sheikh Sultan bin Muhammad al Qasimi, mtawala wa Sharjah, ambaye ametembelea jengo la kitivo hicho na amefahamishwa kuhusu mbinu za kisasa zinazotumika kufunza sayansi za Qur'ani Tukufu.

Aidha alitembelea ukumbi maalumu wa kujifunza kuhifadhi Qur'ani kwa kutumia teknolojia ya kisasa kabisa.

Kitivo cha Qur'ani Tukufu katika Chuo Kikuu cha Al Qasimia huko Sharjah ni cha kwanza cha aina yake katika Umoja wa Falme za Kiarabu.  Kitivo hicho kinalenga kutoa mafunzo ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu, Tajweed na Tafsri ili kuwatayarisha wahubiri waweze kueneza mafunzo ya Qur'ani Tukufu.

3470096

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
HASSANALI HASSANI ALLY
0
0
I love this univesity
captcha