IQNA

Viongozi wa Kiislamu wakutana Kuala Lumpur, Malaysia

21:23 - December 18, 2019
Habari ID: 3472286
TEHRAN (IQNA) – Viongozi wa nchi muhimu za Kiislamu wamekutana Kuala Lumpur, Malaysia kujadili masuala muhimu ya Uliwmengu wa Kiislamu.

Mkutano huo ambao umeanza Jumatano, unahudhuriwa na na mwenyeji, Waziri Mkuu Mahathir Mohammad wa Malaysia, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mkutano huo ambao unamalizika Disemba 21 umehudhuriwa pia na wawakilishi wa nchi 52 ambao wanajadili masuala muhimu ya uliwmengu wa Kiislamu. Walioandaa mkutano huo wanasisitiza kuwa, kikao hicho hakina lengo la kuchukua nafasi ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) bali lengo lake ni la kuchukua maamuzi ya kivitendo kuhusu masaibu ya Waislamu duniani.  

Jumanne kabla ya kuondoka Tehran kuelekea Malaysia, Rais Rouhani alisema kuwa sera za kueleka mashariki na kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na nchi muhimu za bara Asia ni miongoni mwa malengo ya siku zote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mkutano wa Kimataifa wa Kuala Lumpur 2019. Amesema kuwa, mkutano huo utajadili uhusiano wa pande kadhaa katika Ulimwengu wa Kiislamu. Rais Rouhania aliashiria uwezo wa Ulimwengu wa Kiislamu katika masuala mbalimbali ya kijiografia, nishati, jamii kubwa ya watu, viwanda, utamaduni na ustaarabu na kusema: Ugaidi, vita, umwagaji damu, uingiliaji wa nchi za kigeni katika masuala ya ndani ya nchi nyingine na kutokuwepo mazingira mazuri ya ustawi ni miongoni matatizo ya sasa ya Ulimwengu wa Kiislamu. 

3470143

captcha