Ayatullah Mohammad Imami Kashani, katika hotuba zake za Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema, waistikbari na mabeberu daima wanataka kutoa pigo kwa Waislamu na kuongeza kuwa: "Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh lilianzishwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ili kwa njia hiyo waweze kukidhi maslahi yao (haramu)."
Ayatullah Imami Kashani ameendelea kusema kuwa, wasaliti wengi nchini Iraq ambao wanaungwa mkono na maadui wametumia vibaya maadamano ya wananchi wanaodai haki zao na kwa msingi huo wananchi wa Iraq wanapaswa kuwa waangalifu.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran aidha amekosoa muamala mbaya wa serikali ya Nigeria kwa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo na kuongeza kuwa, ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kujitahidi kuhakikisha kuwa Sheikh Zakzaky anaachiliwa huru haraka.