IQNA

ICC kuchunguza jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

11:20 - December 21, 2019
Habari ID: 3472293
TEHRAN (IQNA) – Mwendesha Mashtaka Mkuu katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amesema ataanzisha uchunguzi kamili kuhusu jinai za kivita za utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Hayo yamesemwa Ijumaa na Fatou Bensouda, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC ambaye amebaini: "Nimeweza kuridhika kuwa, kuna sababu za kimsingi za kuanza uchunguzi kuhusu hali ya Palestina."

Ameongeza kuwa: "Kwa kifupi ni kuwa, nimeweza kuridhika kuwa jinai za kivita zimetendwa au zinatendwa katika Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Jerusalem (Quds) Mashariki na Ukanda wa Ghaza."

Bensouda amesema kabla ya kuanza uchunguzi kamili, ataitaka mahakama hiyo ya ICC yenye makao the Hague, kutoa hukumu kuhusu maeneo ya upeo wa mamlaka yake kwa kuzingatia kuwa utawala wa Israel umekataa kuwa mwanachama wa mahakama hiyo ya kimataifa.

Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeunga mkono hatua hiyo ya Bensouda. Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetoa taarifa na kusema: "Palestina inakaribisha hatua hiyo ambayo imechelewa sana ya kuanza kufanya uchunguzi baada ya miaka mitano ya uchunguzi wa awali."

Mwaka 2015, Bensouda alianzisha uchunguzi wa awali kuhusi jinai za kivita za Israel katika ardhi za Palestina baada ya vita vya Ghaza vya mwaka 2014 ambapo Wapalestina  2,251 waliauwa shahidi, wengi wakiwa ni raia.

Utawala haramu wa Israel na muitifaki wake mkuu yaani Marekani zimekataa kujiunga na mahakama hiyo ya kimataifa ambayo ilianzishwa mwaka 2002 ili kuwahukumu watenda jinai na jinai za kivita duniani. Kama ilivyotarajiwa utawala dhalimu wa Israel umepinga vikali hatua ya Bensouda kuanzisha uchunguzi huo.

3865450

captcha