IQNA

Waislamu California wapata idhini ya kujenga msikiti baada ya miaka 13

11:44 - December 21, 2019
Habari ID: 3472294
TEHRAN (IQNA) – Waislamu katika eneo moja la jimbo la California nchini Marekani hatimaye wamepata idhini ya kujenga msikiti baada ya mapambanao ya miaka 13.

Baraza la Wasimamizi wa Kaunti ya Santa Clara hatimaye limeipa idhini Jamii ya Kiislamu ya San Martin idhini ya kujenga msikiti na makaburi ya Waislamu katika eneo lenye ukubwa wa ekari 14.

Waislamu walinunua ardhi hiyo mwaka 2006 wakiwa na nia ya kujenga Kituo cha Kiislamu cha Cordoba ambacho kinajumuisha msikiti, ukumbi wa kijamii na makaburi.

Hatahivyo majirani wenye chuki dhidi ya Uislamu katika eneo la San Martin walipinga vikali mpango huo wakidai kuwa kutakuwa na msongamano mkubwa wa magari, kelele, usanifu majengo usioendana na historia ya eneo hilo na pia madai kuwa makaburi yatachafua mazingira.

Waislamu wamesema wamegharamika dola milioni tatu ili kuhakikisha kuwa Kituo cha Kiislamu cha Cordoba kinajengwa kwa mujibu wa viwango vya jimbo la California.

Mmoja wa wasimamizi wa Kituo cha Kiislamu cha Cordoba Noshaba Afzal asilimia 50 ya wapinzani wana chuki dhidi ya Uislamu na asilimia 50 waliosalia walikuwa na wasiwasi kuhusu uchafuzi wa maji kutokana na makaburi kuwa eneo hilo na msongamano wa magari. Amesema wameweza kutatua kitaalamu masuala yaliyoibuliwa na kwa msingi huo wamepata idhini ya kujenga kituo hicho cha Kiislamu.

3865487

captcha