IQNA

Waislamu Ethiopia walaani hujuma dhidi ya misikiti nchini humo

15:41 - December 24, 2019
Habari ID: 3472298
TEHRAN (IQNA) – Makumi ya maelefu ya Waislamu wameandamana katika miji kadhaa nchini Ethiopia kulaan hujuma za hivi karibuni dhidi ya misikiti katika eneo lenye Wakristo wengi la Amhara kaskazii mwa nchi hiyo.

Wiki iliyopita, misikiti minne iliteketezwa moto na Wakristo waliokuwa na hasira katika mji wa Mota baada ya kanisa kuteketezwa moto na watu wasiojulikana.

Waandamanaji wamelaani kitendo cha kuteketezwa moto misikiti na kutoa wito kwa serikali kuchukua hatua za kulinda misikiti katika eneo hilo ambalo wakazi wake wengi ni Wakristo.

Afisa wa serikali katika eneo la Amhara amesema watu watano wamekamatwa kwa kushukiwa kuhusika na uteketezaji moto misikiti.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook na kusema: "Njama za watu wenye misimamo ya kufurutu ada ya kutaka kuvuruga historia nzuri ya maelewano na kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini mbali mbali ni jambo lisilikuwa na nafasi  katika Ethiopia mpya inayolenga kustawi."

Abiy Ahmed, ambaye amepata Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2019, amelaani  vitendo hivyo na ametoa  wito kwa Waethiopia wote wapendao amani historia ya watu wa nchi hiyo ambao wamekuwa wakiisi kwa pamoja na kwa kuheshimiana.

Waislamu ni karibu asilimia 35 ya watu wote milioni 110 nchini Ethiopia wakiafuatiwa na Wakristo wa Kiorthodoxi ambao ni takribani asilimia 40.

3866185

captcha