IQNA

Mwili wa Sheikh Zakzaky una vipande 43 vya mabaki ya risasi

19:02 - December 28, 2019
Habari ID: 3472311
TEHRAN (IQNA) – Imebainika kuwa mwili wa Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky una vipande vya mabaki ya risasi.

Majibu ya vipimo vipya vya miale ya X-Ray yanaonesha kuwa, "Kuna vipande 43 vya marisau ya risasi ambavyo vimekwama katika upande wa kushoto wa mwili wa Zakzaky." Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Sheikh Zakzaky anahitaji matibabu ya dharura.

Famili ya Sheikh Zakzaky imesema kwenye taarifa kuwa, "Kama inavyoonekana kwenye picha za miale ya X-Ray, moja ya risasi za wanajeshi magaidi liliharibu kikamilifu jicho la Sheikh Zakzaky na kumpofusha."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, makatili wa Kiwahabbi waliolipwa na utawala wa Saudia walifanya juu chini kuhakikisha kuwa wanamuua Sheikh Zakzaky. Historia bila shaka itarekodi upeo wa juu wa ukatili wa Mawahabbi.

Hivi karibuni pia, Daktari wa Sheikh Zakzaky, Nasser Umar Safir alisema kuendelea kuwepo hai mwanaharakati huyo wa Kiislamu licha ya hali yake mbaya ya kiafya ni jambo linalofanana na muujiza.

Alisema kuwa, baada ya kuchunguza mwili na afya ya Sheikh Zakzaky imebainika kuwa, ameathiriwa na kemikali na sumu iliyotokana na zana na vyombo vinavyotumiwa katika jela ya Kaduna.

Itakumbukwa kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky, 66, na mkewe walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati askari wa jeshi la Nigeria walipovamia na kushambulia Hussainiyah iliyoko katika mji wa Zaria. Katika shambulio hilo, Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria wasiopungua 1,000, wakiwemo wana watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi. Sheikh Zakzaky na mke wake walipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na askari wa Nigeria katika tukio hilo.

Baada ya jitihada kubwa, maandamano ya kila pembe na mashinikizo mengi ya ndani na kimataifa, mnamo mwezi Agosti, mahakama ya Nigeria iliruhusu Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe wapelekwe India kutibiwa, lakini kutokana na matatizo na vizuizi vilivyowekwa na maafisa wa usalama walioandamana naye, kiongozi huyo wa kidini pamoja na mkewe waliamua kurudi Nigeria baada ya kukaa India kwa muda wa siku mbili tu pasi na kupatiwa matibabu.

Kabla ya hapo, Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikuwa imefichua kwamba, serikali ya nchi hiyo imekula njama ya kumuua Sheikh Zakzaky kwa kutumia mbinu tofauti ikiwemo ya kumpa sumu.

3867109 

captcha