IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa

Wamarekani katu hawatapata amani baada ya kumua Shahidi Qassem Soleimani

22:10 - January 03, 2020
Habari ID: 3472330
TEHRAN (IQNA) - Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria juu ya kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusisitiza kuwa, Wamarekani katu hawataonja tena ladha ya amani popote duniani kufuatia ukatili huo.

Ayatullah Ahmad Khatami amesema, "Jina la Qassim Soleimani linafungamana na mapambano; mara kwa mara amekuwa akienda katika ncha ya kufa shahidi, lakini Allah Alitaka shujaa huyu anusurike ili alisambaratishe kundi la kigaidi la Daesh (ISIS)."

Ameeleza  bayana kuwa, wafuasi wa Soleimani watafungamana na kuendeleza njia yake, na kwa Rehema za Allah watapata usingizi mwororo mbele ya macho ya Marekani na waitifaki wake.

Ayatullah Ahmad Khatami ameeleza bayana kuwa, "Wamarekani haswa (Donald) Trump wanafahamu fika kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran italipiza kisasi cha damu ya Luteni Jenerali Soleimani."

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa Tehran ameongeza kuwa, tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ubeberu wa dunia ukiongozwa na Marekani umekuwa katika vita vya kijeshi, vya kiuchumi, vya kisiasa na kisaikolojia dhidi ya Iran.

Viongozi wa dunia wakiwemo hata baadhi ya waitifaki wa Marekani wameendelea kukosoa hatua hiyo ya kichokozi ya Marekani, ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani.

3868239

captcha