IQNA

Maandamano Nigeria kulaani kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Soleimani

8:36 - January 04, 2020
Habari ID: 3472332
TEHRAN (IQNA) – Wananchi wa Nigeria wamendamana kulaani jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Kwa mujibu wa taarifa, wananchi wa Nigeria wameandamana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja kulaani hujuma ya kigaidi ya Marekani ambayo pia ilipelekea kuuawa shahidi Abu Mahdi al Muhandes, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha al-Hashdul al-Shaabi, na watu waliokuwa wameandamana nao mapema Ijumaa asubuhi katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad. Waandamanaji walsikika wakitoa nara za 'Mauti kwa Marekani' na 'Mauti kwa Israel' katika maandamano hayo.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria aidha imetoa tamko na mbali na kuilaani Marekani kwa kumuua kigaidi Kamanda Qassem Soleimani, imelipa mkono wa pole taifa na serikali ya Iran na kusisitiza kuwa, ugaidi huo wa Marekani ni jinai isiyosameheka.

Nchi, taasisi, vyama na shakhsia mbalimbali duniani wanaendelea kulaani jinai hiyo ya Marekani ya kumuua shahidi Meja Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ametoa amri ya kuuliwa shahidi Jenerali Qassem Soleimani.  

7195925

captcha