IQNA

Kiongozi wa HAMAS Ismail Hania ahutubu katika mazishi ya Kamanda Soleimani; amtaja kuwa ni shahidi wa Quds Tukufu

14:33 - January 06, 2020
Habari ID: 3472341
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amefika Tehran kushiriki katika shughuli ya mazishi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na mashahidi wenzake.

Akihutubu mbele ya mamilioni ya waombilezaji ametilia mkazo wajibu wa kuendelea na muqawama au mapambano hadi ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa.
Aidha alisisitiza kuwa, mwamko wa muqawama katika ardhi za Palestina utaendelea na mapambano ya kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni na za rais wa Marekani yatazidi kasi hadi ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa.
Ismail Hania aidha amesema, Luteni Jenerali Soleimani alipitisha uhai wake wote katika kuunga mkono taifa la Palestina na Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa na kusisitiza mara tatu kwamba Shahidi Soleimani ni shahidi wa Quds.
Mkuu huyo wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS aidha amelaani jinai ya Marekani na utawala wa Kizayuni ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Soleimani na kusisitiza kuwa, ushindi wa kambi ya muqawama uliopatikana huko Lebanon na Ghaza bila ya shaka yoyote umetokana na juhudi za Luteni Jenerali Soleimani na bila ya shaka yoyote kambi ya Muqawama itapata ushindi mkubwa pia katika mapambano muhimu mno yajayo.
Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq al Hashd al Shaabi pamoja na wenzao wengine wanane waliuliwa shahidi usiku wa kuamika Ijumaa tarehe tatu Januari 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na utawala wa kigaidi wa Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq.

3869559

captcha