IQNA

Msongamano mkubwa katika Maziko ya Shahidi Qassem Soleimani

16:28 - January 07, 2020
Habari ID: 3472347
TEHRAN (IQNA) – Shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani amezikwa kwa kuchelewa kufuatia msongamano mkubwa katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa Iran.

Aidha taarifa zinasema watu wasiopungua 32 walifariki dunia mjini Kerman, Iran na makumi ya wengine walijeruhiwa katika mkanyagano kwenye shughuli ya maziko ya shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani pamoja na ashahidi mwingine wa muqawama kutoka mji huo wa Kerman.

Umati wa mamilioni ya watu uliojitokeza leo katika mji wa Kerman kwa ajili mazishi ya Luteni Jenerali shahidi Qassim Soleimani umekwamisha kabisa shughuli ya maziko.

Kamati ya mazishi ya shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani imetangaza kuwa, maziko hayo yameakhirishwa kutokana na umati mkubwa wa watu kwani hali ilivyo haiwezekani kuwazika mashahidi hao kwa leo. Taarifa hiyo imeeleza kwamba, kutatolewa taarifa baadaye kuhusiana na ratiba ya maziko hayo.

Takriban Wairani milioni saba walikusanyika jana katika mji mkuu wa Iran, Tehran kuuaga mwili wa Jenerali Soleimani pamoja na mashahidi wenzake kabla ya kuelekea katika mji mtakatifu wa Qum. Matembezi ya kumuomboleza na kumuenzi Haji Soleimani na mashahidi wenzake yalifanyika pia katika miji ya Baghdad, Karbala, Najaf nchini Iraq na kisha nchini Iran katika miji ya Ahwaz, Mashhad, Tehran na Qum kabla ya kufika mjini Kerman.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine nane, walishambuliwa kwa anga na wanajeshi vamizi na wa kigaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote walikufa shahidi katika tukio hilo.

3869821

captcha