IQNA

Baraza la Kiislamu Marekani lawataka Wairani Wamarekani wachukue tahadhari

17:21 - January 07, 2020
Habari ID: 3472349
TEHRAN (IQNA) – Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limetoa ushauri kwa Wairani-Wamarekani (Wairani wenye uraia wa Marekani) baada ya kubainika kuwa wanasumbuliwa na kubaguliwa na maafisa wa usalama kufuatia matukio ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi.

Katika taarifa, CAIR imesema zaidi ya Wairani-Wamarekani wapatao 60 wameshikiliwa na kusailiwa kwa masaa kadhaa katika Uwanja wa Ndege wa Jimbo la Washington walipokuwa wakirejea Marekani baad aya kuhudhuria tamasha ya utamaduni wa Iran katika nchi jirani ya Canada.

CAIR, ambayo hutetea haki za Waislamu nchini Marekani, imesema imewapa muongozi Wairani-Wamarekani kuhusu haki zao huku hali ya taharuki ikiendelea. CAIR imesema inakusanya malalamiko ya watu ambao walisimamishwa katika unwaja na ndege na kusailiwa kwa sababu tu ni Wairani-Wamarekani.

Muirrani Mmarekani ambaye anafanya kazi na CAIR na ambaye wakati moja aliwahi kuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Georgia anasema baada ya Marekani kumuua kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani,  familia za Wairani-Wamarekani, ikiwemo familia yake, zimekumbwa na masaibu makubwa.

"Tunahisi hali hii katika maisha yetu yote," amesema Dkt. Abbas Barzegar. "Familia zetu zimeathiriwa, tumebadilisha ratiba za usafiri. Watu wana wasiwasi kuwa visa zao zitabatilishwa, au green card zao zitabatilishwa, au watakamtwa na kufungw ajela bila sababu," amesema.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine nane, walishambuliwa kwa anga na wanajeshi vamizi na wa kigaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote walikufa shahidi katika tukio hilo.

Kufuatia ugaidi huo Marekani, Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, imepitisha muswada wa sharia ambao umeitaja Wizara ya Ulinzi wa Marekani, na mashirika yake yote, kuwa ni kundi la kigaidi.

3470291

captcha