IQNA

Msikiti wa Quebec Canada wakarabatiwa

9:19 - January 16, 2020
Habari ID: 3472376
TEHRAN (IQNA) – Msikiti wa Quebec Canada unaendelea kukarabatiwa ili kuwawezesha Waislamu wa mji huo kupata eneo salama la ibada.

Kwa mujibu wa taarifa, msikiti huo ambao uko katika Manispaa ya Sainte Foy unafanyiwa ukarabati mkubwa ambao unatazamiwa kugharimu dola milioni 1.2 na hivyo kuweza kutumiwa na idadi kubwa ya Waislamu wanaoongezeka mjini humo.

Huu ni msikiti ambao mnamo Januari 29 2017 ulihujumiwa na magaidi ambapo  Waislamu sita waliuawa katika hujuma ya kigaidi. Magaidi waliwafyatulia risasi Waislamu waliokuwa katika msikiti wa Kituo cha Kiutamaduni cha Quebec, wakati wa Sala ya Ishaa saa mbili usiku.

Mwenyekiti wa zamani wa msikiti huo Mohamed Labidi anasema mpango wa kuukarabati msikiti ulikuwepo hata kabla ya hujuma hiyo ya kigaidi lakini baada ya tukio hilo mchakato huo ulishika kasi zaidi.

Kwa ujumla Canada ni nchi ambayo huwakaribisha wahamiaji na wafuasi wa dini zote lakini eneo linalozungumza kifaransa la Quebec limekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu kuwakubali watu wa rangi na dini mbali mbali.

3470370

captcha