IQNA

Televisheni na Redio za Aceh, Indonesia zatakiwa kurusha hewani adhana

11:38 - January 19, 2020
Habari ID: 3472385
TEHRAN (IQNA) – Uongozi wa mkoa wa Aceh nchini Indonesia umepitisha sheria ya kuzitaka stesheni zote za televisheni na radio nchini humo kurusha hewani adhana ukiwadia wakati wa sala.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, uamuzi huo umechukuliwa na Baraza la Vyombo vya Habari katika mkoa huo ulio magharibi mwa Indonesia.

Baraza hilo limesema uamuzi huo unalenga kustawisha thamani za kidini na sheria za Kiislamu na hivyo kituo chochote cha televisehni au redio kitakachokiuka uamuzi huo kitatozwa faini.

Jimbo la Aceh nchini Indonesia lina mamlaka ya ndani ya kujitawala na linaongoza katika uktekelezwaji wa sheria za Kiislamu nchini Indonesia.

Nchi ya Indonesia iko kusini Mashariki mwa Asia na ina idadi ya watu milioni 264 ambapo milioni 225 ni Waislamu na hivyo kuifanya kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani.

3872567

captcha