IQNA

Askari wa utawala wa Kizayuni waua Wapalestina 3 Ghaza

16:15 - January 22, 2020
Habari ID: 3472396
TEHRAN (IQNA) - Wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua shahidi kwa kuwapiga risasi Wapalestina watatu katika uzio wa Ukanda wa Ghaza.

Vyombo vya habari vya utawala huo haramu vimeripoti kuwa, Wapalestina hao waliuawa usiku wa kuamkia leo eti kwa kujaribu kuvuka mpaka na kuingia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Msemaji wa jeshi la Israel anadai kuwa, Wapalestina hao waliingia Israel baada ya kuvuka mpaka wa Ghaza na kuwarushia vilipuzi wanajeshi wa utawala huo ghasibu.

Kwa mujibu wa Jumuiya ya Taifa ya Familia za Kipalestina, Wapalestina 149 waliuawa shahidi na askari wa utawala haramu wa Israel mwaka uliopita wa 2019, ambapo asilimia 74 miongoni mwao walikuwa wanatoka Ukanda wa Gaza.

Mohammed Sbeihat, Katibu Mkuu wa taasisi hiyo ya kutetea haki za Wapalestina amesema kuwa, asilimia 23 ya Wapalestina waliouawa shahidi ni watoto wadogo.

Mauaji haya yanaendelea katika hali ambayo, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stéphane Dujarric amesema kuwa umoja huo utaendelea kushughulikia mahitaji ya kibinadamu ya Wapalestina katika ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu na Israel na kutafuta suluhisho la muda mrefu ikiwa ni pamoja na kukomesha mzingiro wa Ghaza.

Hayo yanaripotiwa wakati ambao, Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina 149 katika mwaka uliopita wa 2019, aghalabu wakiwa katika Ukanda wa Ghaza.

Mohammed Sbeihat, Katibu Mkuu wa Mjumuiko wa Kiataifa wa Familia za Mashahidi wa Palestina amesema: "Wapalestina waliouawa na wanajeshi wa utawlaa wa Israel mwaka 2019 ni 149 ambapo 112 ni kutoka Ukanda wa Ghaa na 37 ni kutoka Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan."

Katibu Mkuu wa Mjumuiko wa Kiataifa wa Familia za Mashahidi wa Palestina pia amesema kwa ujumla katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Wapalestina 807 waliuawa shahidi na Israel hii ikiwa ni wastani wa watu 161 kwa mwaka.

Wapalestina wanapigania ukombozi wa ardhi zao ambazo zinaendelea kukaliwa kwa mabavu na utawala bandia wa Israel.

3873433

captcha