IQNA

Mwanamke wa kwanza mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu Uingereza

13:15 - January 23, 2020
Habari ID: 3472398
TEHRAN (IQNA) – Baraza la Shura (Mashauriano) la Jumuiya ya Waislamu Uingereza limemchagua Bi. Raghad Al Tikriti kuwa mwenyekiti wake mpya.

Kabla ya nafasi yake mpya, Bi. Al Tikriti alikuwa Naibu Mwnyekiti na Mkuu wa Vyombo vya Habari vya jumuyiya hiyo na hivyo anafahamu shughuli za uendeshaji wake.

Baraza la Waislamu Uingereza (MAB) limekaribisha chaguzi wa Bi. Al Tikriti na kuutaja kuwa wa kihistoria.

Baada ya kuchaguliwa Bi. Al Tikriti alisema: "Ni fahari kubwa kuchaguliwa  kuwa mwanamke wa kwanza mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu Uingereza ili kuwakilisha na kuhudumua wanachama wetu kote nchini."

Jumuiya ya Waislamu Uingereza ilianzisha mwaka 1997 kwa lengo la kuwahimia Waislamu kushiriki kikikamilifu katika harakati za jamii nchini Uingereza na ili kuwawezesha kuwa raia wenye kuthaminiwa katika nchi hiyo ya Ulaya.

Aidha jumuiya hiyo hushirikiana an wadai wengine kusuluhisha matatizo yanayozikumba jamii za Waislamu kama vile uhalifu, kufeli kielimu, kuenea ubaguzi na chuki dhidi ya Waislamu n.k.

Inakadiriwa kuwa kuna Waislamu milioni tatu nchini Uingerereza kati ya watu milioni 66 nchini humo. Waislamu wameenea katika maeneo yote ya Uingereza na wamewakilishwa katika sekta zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Waislamu wanamiliki migahawa, na biasahra nyinginezo na pia wanafanya kazi katika sekta za sheria, tiba, teknolojia, usafiri, elimu, vyombo vya habari, sanaa, mitindo n.k. Aidha Waislamu ni kati ya wanamichezo na wanariadha bora Uingereza.

Waislamu wa kwanza kuwasili Uingereza kama kundi walifika nchini humo karne ya 18 kama mabaharia maarufu kama lascars kutoka Bara Hindi. 

3470428

captcha