IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Sera ovu na ya kishetani ya Marekani kuhusu Palestina haitafanikiwa

19:38 - January 30, 2020
Habari ID: 3472421
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pendekezo la Marekani lililopewa jina la 'Muamala wa Karne' katu halitazaa matunda kwa Rehema za Mwenyezi Mungu.

Katika ujumbe uliotumwa kwenye ukurasa wa Twitter, Ayatullah Ali Khemenei amesema, "kwa mshangao mkubwa kwa wanasiasa wa Marekani, sera ovu na ya kishetani ya Wamarekani kwa Palestina-hicho kinachoitwa #Muamala wa Karne- kamwe hauwezi kuzaa matunda yoyote kwa Rehema  za Allah."

Katika ujumbe huo na huku akikosoa vikali pendekezo la Marekani la kutaka kuyahudishwa Quds Tukufu iwe mikononi mwa Mayahudi, Kiongozi Muadhamu amesema wazo hilo ni la kipumbavu na lisilokuwa na mantiki yoyote.

Ayatullah Ali Khemenei amesisitiza kuwa, kadhia ya Palestina kamwe haiwezi kusahaulika na bila shaka mataifa ya Kiislamu yatasisima kidete kuhakikisha kuwa ndoto za Muamala wa Karne hazifikiwi.

Juumanne na Rais Donald Trump wa Marekani akiwa pamoja na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu wa lsrael walizindua mpango wa eti amani kati ya Palestina na Israel uaojulikana pia kama 'muamala wa karne'. Kikao cha uzinduzi wa mpango huo pia kilihudhuriwa na mabalozi wa baadhi ya nchi vibaraka za Kiarabu.

Mpango huo wa Marekani ambao unautambua mji mtakatifu wa Quds kuwa mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel na kupuuza moja kwa moja haki za kimsingi za wakaazi asilia wa mji huo, unathibitisha wazi kuwa umebuniwa kwa madhumuni ya kulinda maslahi haramu ya utawala huo na kudhamini usalama wake unaolegalega.

3470476

captcha