IQNA

Msikiti wa kwanza kabisa wafunguliwa nchini Slovenia

17:42 - February 04, 2020
Habari ID: 3472439
TEHRAN (IQNA) - Msikiti wa kwanza kabisa katika historia ya Slovenia umefunguliwa Jumatatu katika mji mkuu, Ljubljana baada ya Waisalmu kuvuka vizingiti ya kifedha na upinzani wa watu wenye mismamo mikali ya mrengo wakulia.

Msikiti huo umefunguliwa baada ya kupita miaka 50 tokea litolewa ombi la kutaka eneo hilo la ibada lijengwe. Wapinzani wa mradi huo wamekuwa wakitumia kila mbinu kupinga ujenzi wa msikiti huo ikiwa ni pamoja na kuweka vichwa vya nguruwe katika ardhi  ya msikiti huo. Aidha wapinzani wa msikiti huo walipinga vikali hatua ya Qatar kufadhili ujenzi wake wakidai kuwa nchi hiyo inaunga mkono ugaidi.

Mkuu wa Jamii ya Kiislamu Slovenia Mufti Nedzad Grabu amesema ujenzi wa msikiti huo ni tukio la kihistoria kwa maisha ya Waislamu.

"Slovenia ni nchi ya mwisho ya Yugosalvia ya zamani kupata msikiti," amewaambia waandishi habari.

Waislamu wa Slovenia, ambayo aghalabu ya wakaazi wake ni Wakatoliki, waliwasilisha pendekezo la ujenzi wa msikiti miaka 50 iliyopta wakati Slovenia ilikuwa bado ni sehemu ya Yugosalvia ya Kikomunisti.

Hatimaye miaka 15 iliyopita Waislamu walipata kibali cha kujenga msikiti lakini ujenzi huo ulipingwa vikali na wanasiasa wa mrengo wa kulia wenye misiammo ya kufuruta na pia kulikuwa na tatizo la ufadhili.

Hatimaye ujenzi ulianza mwaka 2013 ambapo mradi huo umegarimu Euro milioni 34 huku Qatar ikitoa mchango wa Euro milioni 28. Msikiti huo una uwezo wa kubeba waumini 1,400 na pia una kituo cha Kiislamu kinachojumuisha kitengo cha masomo, maktaba, mgahawa, uwanja wa basketboli na nyumba ya imamu.

Waislamu wanakadiriwa kuwa ni asilimi 2.5 kati ya watu wote milioni mbili nchini humo ambapo idadi yao inakadiriwa kuwa ni 80,000.

Slovenia ni nchi ya Ulaya ya Kati, mashariki kwa milima ya Alpi. Imepakana na Italia, Ghuba ya Adria ya Bahari ya Mediteranea, Kroatia, Hungaria na Austria na ni mwanachama wa wa Umoja wa Ulaya.

3876388

captcha