IQNA

Maoni

Taathira ya Waislamu katika uchaguzi wa rais Marekani

16:04 - March 03, 2020
Habari ID: 3472525
TEHRAN (IQNA) –Waislamu nchini Marekani wanatazamiwa kuwa na taathira kubwa katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Bi. Rashmee Roshan Laa, mwandishi habari Muingereza mwenye asili ya India ambaye pia ni mtaalamu wa siasa za Marekani anasema: "Masuala yanayohusu sera za kigeni za serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani na matamshi yake ya kibaguzi ni nukta ambazo zimepelekea Waislamu waunge mkono chama cha Democrat. Hivi sasa Trump amepoteza umaarufu wake ambao sasa umefika chini ya asilimia 50 nchini Marekani."

Katika mahojiano maalumu na IQNA, Bi. Roshan Laal amesema kuwa sera za kibaguzi za Trump hasa uamuzi wake wa kuwapiga marufuku raia wa nchi ambazo aghalabu ni za Kiislamu (Somalia, Syria, Iran, Iraq, Libya, Sudan na Yemen) kuingia Marekani ni nukta ambayo imepelekea waliowachache nchini  humo, hasa Waislamu waazimie kupiga kura katika uchaguzi ujao wa rais.

Akijibu swali ni kwa nini Trump ana uhusiano mzuri na Saudi Arabia lakini wakati huo huo anawapiga marufuku raia wa nchi kadhaa za Kiislamu kuingia Marekani, Bi Roshan Laal anasema hakuna mantiki maalumu iliyotumiwa katika kuwapiga amrufuku raia wan chi za Kiislamu kuingia Marekani. Aidha anasema hakuna raia wa nchi hizo zilizopigwa marufuku aliyewahi kutekeleza hujuma ya kigaidi Marekani katika kipindi cha miaka 40 hasa katika tukio la Septemba 11.

Aidha anasema katika mchuano wa kuteua mgombea wa chama cha Democrat katika uchaguzi wa rais, inaelekea kuwa Bernie Sanders ana nafasi bora zaidi ya kupeperusha tiketi ya chama hicho.

3882102

captcha