IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani yafanyika Ufilipino

10:28 - March 05, 2020
Habari ID: 3472532
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 46 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu yamefanyika nchini Ufilipino ambapo rais Rodrigo Duterte wa nchi hiyo amewatumia washiriki ujumbe maalumu.

Katika ujumbe wake, Rais Duterte amewatumia salama za heri na fanaka Waislamu wa Ufilipino na ameishukuru Tume ya Kitaifa ya Waislamu wa Ufilipino kwa kuandaa mashindano hayo. Aidha ameelezea matumaini yake kuwa Waislamu wa Ufilipino watakuwa ambalozi wazuri wa nchi yao duniani.

Akizungumza katika mashindano hayo, Katibu Mkuu wa  Tume ya Kitaifa ya Waislamu wa Ufilipino Saidamen Balt Pangarungan amewasilisha ripoti kuhus mashindano hayo na kuelekeza matumainikuwa yataweza kustawisha ufahamu wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

Mashindano hayo ya kusoma Qur'ani yalikuwa na washiriki 36 wa kike na kiume. Tume ya Kitaifa ya Waislamu wa Ufilipino ni taasisi ya kiserikali yenye lengo la kutetea haki za Waislamu nchini humo.

3883102

captcha