IQNA

Mgahawa wa Bunge la Uingereza kuanza kuuza chakula Halali

17:40 - March 15, 2020
Habari ID: 3472568
TEHRAN (IQNA)- Bunge la Uingereza, House of Commons, litaanza kuuza chakula Halali, ambacho kimetayarishwa kwa misingi ya mafundisho ya Kiislam, kuanzia Machi 30 kufuatia ombi la wabunge Waislamu.

Aidha bunge hilo limesema litatayarisha chakula kwa msingi wa dini ya Kiyahudi ambacho ni maarufu kama Kosher. Hatua hiyo pia inafuatia ombi la wabunge Mayahudi.

Mpango huo utatekelezwa kwa majaribio kwa muda wa miezi mitatu na iwapo kutakuwa na wanunuzi wa kutosha, basi hatua hiyo itakuwa ya daima.

Bunge la Uingereza limechukua uamuzi huo baad aya barua ya pamoja ya mbunge Muislamu wa chama cha upinzani cha Leba Zahra Sultana na mbunge Myahudi pia wa chama cha Leba Charlotte Nicols.

Hivi sasa kuna wabunge 19 Waislamu katika Bunge la Commons mbali na wafanyakazi Waislamu katika bunge hilo ambao watanufaika na uamuzi huo.

Kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni ya watu Uingereza, kuna Waislamu milioni 2.8 nchini humo kati ya watu milioni 64 nchini humo. Waislamu wameenea katika maeneo yote ya Uingereza na wamewakilishwa katika sekta zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Waislamu wanamiliki migahawa, na biasahra nyinginezo na pia wanafanya kazi katika sekta za sheria, tiba, teknolojia, usafiri, elimu, vyombo vya habari, sanaa, mitindo n.k. Aidha Waislamu ni kati ya wanamichezo na wanariadha bora Uingereza.

Waislamu wametoa mchango mkubwa katika kuifanya Uingereza iwe nchi yenye watu wa makabila na dini mbali mbali. Karibu asilimia 47 ya Waislamu Uingereza wamemzaliwa nchini humo. Kuna Waislamu 290,000 walio na umri wa kati ya miaka 9-14 huku asilimia 53 ya Waislamu wakiwa chini ya umri wa miaka 19.

3470910

captcha