IQNA

Hofu ya corona

Amri kali ya kutotoka nje usiku na mchana kutekelezwa Makka na Madina

19:17 - April 02, 2020
Habari ID: 3472627
TEHRAN (IQNA) – Saudi Arabia imetangaza sheria kali ya kutotoka nje katika miji mitakatifu ya Makka na Madina ikiwa ni sehemu za mkakati wa utawala huo wa kifalme kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imesema sheria hiyo ya kutotoka nje masaa 24, yaani usiku na mchana, itatekeelzwa katika mjiji mitakatifu ya Makka na Madina na ni watu wazima tu ndio watakaoruhusiwa kwenda nje ya nyumba kwa ajili ya shughuli ya dharura ya kununua dawa au chakula baina ya saa 12 asubuhi hadi saa tisa mchana. Aidha katika muda huo maeneo mengine yatakayotoa huduma ni benki na vituo vya petroli.

Amri hiyo ya kutotoka nje kikamilifu imeanza kutekelezwa leo Alhamisi kwa muda usiojulikana. Watakaoruhusiwa kufanya kazi katika miji hiyo miwili ni wale walioajiriwa katika maeneo muhimu ya sekta za umma na binafsi.

Aidha sheria hiyo imesema kila gari itaruhusiwa kuwa na dereva na abiria moja tu katika miji hiyo miwili.  Mnamo Machi 25 Saudi Arabia ilitangaza sheria jumla ya kutotoka nja usiku kitaifai ikiwa ni pamoja na kuzuia kuingia na kutoka Makka, Madina, na Riyadh na pia marufuku ya safari katika mikoa 13 nchini humo. Hadi sasa watu 1,700 wameambukizwa ugonjwa wa COVID-19 nchini Saudia huku wengine 19 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

3888702

captcha