IQNA

Barua ya Mkuu wa vyuo vya kidini Iran kwa Papa Francis kuhusu corona

7:39 - April 05, 2020
Habari ID: 3472634
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa vyuo vya kidini katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia barua Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, na kusema vyuo vya kidini Iran viko tayari kubadilishana uzoefu na vyuo vya kidini na viongozi wa dini za mbinguni kote duniani.

Kwa mujibu wa tovuti ya hawzahnews Ayatullah Alireza Arafi, mkurugenzi wa vyuo vya kidini Iran amemuandikia barua Papa Francis na kutangaza kufungamana na watu wa dini zote na mataifa yote ambao wamepatwa na msiba na kuathiriwa na ugonjwa wa corona.

Katika barua yake, Ayatullah Arafi ameongeza kuwa: "Katika mantiki ya dini za mbinguni, maafa na balaa za kimaumbile ni mtihani ambao huandaa mazingira ya kukamilika mwanadamu na fursa ya kustawi na kunawiri roho ya mshikamano na kujitolea."

Aidha Mkuu wa vyuo vya kidini katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika barua hiyo kuhusu udharura kuimarisha misingi ya kiitikadi na kuzingatia utakasaji wa nafsi na roho pamoja na kuilinda jamii ili isikumbwe na machafu au maovu. Pia ameashiria uwezo wa milele wa Mwenyezi Mungu SWT na kukumbusha kuwa: "Kukabiliana na changamoto iliyopo na migogoro mingine ya zama za sasa kama vile ukosefu wa uadilifu, vikwazo vilivyo dhidi ya binadamu, mgogoro wa mazingira, vita, na ugaidi yote yanahitaji kutafakari pamoja na ushirikiano wa kimataifa."

894151

captcha