IQNA

Mualamaa wa Kiislamu duniani wataka Zaka itumike katika vita dhidi ya corona

11:40 - April 11, 2020
Habari ID: 3472654
TEHRAN (IQNA)- Maimamu na wanafikra kadhaa wa Kiislamu na Kiarabu duniani wametia wametoa wito wa kutaka Zaka itumike katika jitihada za kukabiliana na janga la ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa tovuti ya RT Arabic, katika taarifa hiyo ya maimamu, na wanafikra katika taasisi za Kiislamu na Kiarabu wamesema Zaka inayotolewa na Waislamu duniani ni takribani dola billion 400 katika ulimwengu wa Kiislamu.

Wameongeza kuwa kwa kuzingatia vizingiti vilivyowekwa katika nchi nyingi ili kuzuia kuenea corona, Zaka inawezaaa kutumika kuwasaidia watu ambao maisha yao yameathirika kutokana na janga la corona.

Wiki iliyopita, Mufti wa Mji wa Quds (Jerusalem) Sheikh Ekrima Sabri alitoa Fatwa na kusema Zaka inaweza kutumika katika vita dhidi ya corona.

Sheikh Sabri ambaye pia ni mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu na Imamu wa Msikiti wa Al-Aqsa mjini humo alitoa wito kwa Waislamu wanaojiweza kutumia Zaka yao kuwasaidia walioathirika kiuchumi na corona.

Aliongeza kuwa hakuna  haja ya kusibiri Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uwadie ili kutoa Zaka kwa kuzingatia mazingira ya sasa duanini.

Aidha aliwapongeza na kuwashukuru Waislamu ambao tayari wameanza kuwasaidia walioathirika na janga la COVID-19.

Takribani watu milioni 1.7 wameabukizwa corona duniani kufikia sasa huku waliofariki wakizidi laki moja. Ili kuzuia kuenea corona, serikali nyingi zimewataka watu wakae majumbani mwao hali ambayo imewafanya watu wengi ambao ni vibarua na wanaotegemea biashara ndogo kukosa fedha za kujimudu kimaisha.

3890584

captcha