Kwa mujibu wa taarifa, Mohammad al Aqil, afisa mwandamizi wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu Saudi Arabia katika mahojiano na Televisheni ya Al Saudiya katika kujibu swali kuhusu iwapo kusitishwa kwa sala za jamaa misikiti pia kutahusisha sala ya Tarawih katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani amesema: “Maadamu hakuna amri kutoka baraza kuu la ulamaa na taasisi husika kuhusu kuondoa marufuku ya sala za jamaa, basi marufuku ya sala za jamaa itaendelea.”
Naye Ahmad al Mansouri, mjumbe wa mkuu wa masuala ya Harameini (Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina) ametoa kauli kuhusu sala katika maeneo hayo mawili matakatifu na kusema: “Kamati kuu itafanya tathmini kuhusu kuswaliwa Sala ya tarawih katika Msikiti Mtakatifu wa Makka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.”
Hadi kufikia Jumamosi 10 Aprili, watu 3,651 walikuwa wameambukizwa corona nchini Suadia Arabia na miongoni mwaka 47 wameaga dunia.