IQNA

Kamati ya Fiqhi Amerika Kaskazini yatangaza Aprili 24 kuwa Ramadhani Mosi

12:57 - April 12, 2020
Habari ID: 3472659
TEHRAN (IQNA) – Baraza la Fiqhi ya Amerika Kaskazini imetangaza kuwa Ijumaa Aprili 24 itakuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa baraza hilo, mahesabu ya kifalaki yanaashiria kuwa, mwezi mwandamo utaonekana Aprili 23, 2020 saa nane na dakika 27 kwa mujibu wa saa za UTC. Taarifa hiyo imesema mwezi mwandamo utaonekana katika eneo zima la Amerika Kaskazini na Kusini na kwa msingi huo Ramadhani Mosi 1441 itakuwa sawa na Ijumaa Aprili 24, 2020 katika eneo hilo.

Baraza la Fiqhi la Amerika Kaskazini linasema katika tovuti yake kuwa ni taasisi inayowaleta pamoja wasomi za Kiislamu kutoka Marekani na Canada.

Baraza hilo halitegemei msingi wa Sunna ya kuuona mwezi mwandamo kwa macho au kwa teleskopu bali hutegemea mahesabu ya kifalaki na kwa msingi huo limetabiri pia kuwa Mei 24, 2020, itakuwa tarehe mosi Shawwal 1441 na hivyo ni siku kuu ya Idul Fitr. Baraza la Fiqhi la Amerika Kaskazini linasema mbinu ya kutegemea mahesabu ya kifalaki inakubalika kwa mujibu wa sheria za Kiislamu

3471101

captcha