IQNA

Waislamu Marekani wachanga kuwasaidia maimamu wa misikiti wakati wa corona

23:38 - April 20, 2020
Habari ID: 3472685
TEHRAN (IQNA)- Viongozi wanne maarufu wa jamii ya Waislamu nchini Marekani wanachangisha fedha za kuwasiaidia maimamu na wafanyakazi wa misikiti katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa corona au COVID-19 nchini humo.

Mchakato huo hadi sasa umechangisha US$ 167,000 kwa ajili ya kuwalipa maimamu na wafanyakazi wa misikiti.

Mpango huo umeanzishwa na jumuiya moja ya Waislamu ya kuchangisha pesa kupitia intaneti inayojulikana kama LaunchGood, Wakfu wa Jamii ya Waislamu Marekani na viongozi wanne maarufu wa jamii ya Waislamu ambao ni Imam Zaid Shakir, Imam Omar Suleiman, Imam Yasir Qadhi, na Imam Suhaib Webb.

Aghalabu ya misikiti hutegemea fedha ambazo huchangwa wakati wa Sala ya Ijumaa au michango ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kwa kuzingatia kuwa misikiti imefungwa kwa wiki kadhaa sasa na pia itaendelea kufungwa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na janga la corona, imekuwa vigumu kwa maimamu na wafanyakazi wa misikiti na kujimudu kimaisha.

Imam Yasir Qadhi amesisitiza kuwa, Waislamu hawapaswi kupuuza taasisi za kidini hasa misikiti na viongozi wao wa kidini wakiwemo maimamu, mashekhe na wahubiri katika kipindi hiki cha janga la corona.

3471210

captcha