IQNA

Marufuku ya umma kuswali katika Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina

15:48 - April 21, 2020
Habari ID: 3472689
TEHRAN (IQNA)- Msikiti Mtakatifu wa Makka (al-Masjid al-Ḥaram) na Msikiti Mtakatifu wa Mtume SAW (Al Masjid an Nabawi) mjini Madina, itaendelewa kufungwa kwa umma kwa ajili ya swala za jamaa hadi mwisho wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa ujumbe wa Twitter wa mfawidhi wa misikiti hiyo miwili mitakatifu Abdulrahman bin Abdulazizi al-Sudais, uamuzi huo umechukuliwa na wakuu wa Saudia ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona au COVID-19. Amesema swala ya Tarawih itaswaliwa katika misikiti hiyo miwili pasina kuhudhuriwa na umma na kwamba watakaoshriki ni wafanyakazi tu.

Aidha amesema Itikafu katika hiyo miwili mitakatifu pia ni marufuku kabisa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Kati kati ya mwezi Machi Saudi Arabia ilipiga marufuku sala zote tano na sala za Ijumaa katika misikiti yote nchini humo ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19. Aidha Ibada ya Umrah imesimamsihwa kwa muda baada ya kufungwa Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina.

Hadi kufikia Aprili 21,  watu walioambukizwa COVID-19 nchini Saudi Arabia ni 10,487 na waliofarikia ni 103, ikiwa ni idadi kubwa zaidi miongozi mwa nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.

3893058

captcha