IQNA

Mafunzo ya usomaji Qur’ani kupitia intaneti nchini Tunisia

19:39 - April 29, 2020
Habari ID: 3472716
TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Utamaaduni cha Jamhuri ya Kiislamu Iran nchini Tunisia kimeandaa mafunzo ya usomaji Qur’ani Tukufu kwa njia ya intaneti katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), masomo hayo ni kuhusu misingi ya sawt, lahn na tajwid katika usomaji Qur’ani. Aidha washiriki wanajifunza kuhusu tafsiri ya aya za Qur’ani Tukufu.

Masomo hayo yanafanyika kwa njia ya intaneti kupitia jukwaa la WhatsApp na waalimu katika kozi hiyo ni Qarii Sayyid Jasim Mousawi na Sayyed Hassan Esmati ambao wanatoa mafunzo kwa lugha Kiarabu na Kifaransa ambazo hutumika Tunisia

Mafunzo hayo ya Qur’ani mwaka huu yamefanyika kwa njia ya intaneti katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na vizingiti vilivyowekwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

3894986

captcha