IQNA

Swala za jamaa zaanza katika misikiti Syria

15:46 - May 27, 2020
Habari ID: 3472808
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu ya Syria imetangaza kuanza swala za jamaa katika misikiti ya nchi hiyo kuanzia sikua ya Jumatano.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Wizara ya Wakfu ya Syria imetoa taarifa kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema, misikiti  nchini humo sasa itakuwa na idhini ya kuendeleza Swala za jamaa ikiwa ni pamoja na Swala ya Ijumaa .

Wizara ya Wakfu ya Syria imesisitiza kuwa wale wote wanaofika katika misikiti watawajibika kuzingatia kanuni zote za afya ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Syria, sawa na aghalalbu ya nchi katika ulimwengu wa Kiislamu ilikuwa imefunga misikiti yake kwa zaidi ya miezi miwili ili kuzuia kuenea ugonjwa wa  COVID-19.

Hadi kufikia  Mei 26 watu milioni 5,606,220 walikuwa wameambukizwa COVID-19 duniani kote huku wengine 348,248 wakiwa wameaga dunia. Marekani ndiyo nchi iliyoathiriwa vibaya zaidi na ugonjwa huo duniani ambapo idadi ya walioambukizwa ni 1,706,226 na waliofariki dunia wanakaribia laki moja. Ugonjwa wa COVID-19 uliripotiwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2019 katika mji wa Wuhan nchini China na baada ya hapo sasa umeenea katika kila kona ya dunia.

3901436

 
captcha