Uwezo wake wa kusoma Qur'ani kwa ustadi uligunduliwa na Sheikhe mmoja wakati akiwa bado katika shule ya msingi.
Alihimizwa sana na Sheikhe huyo kuimarisha kipaji chake cha qiraa ya Qur'ani Tukufu sambamba na kutafakari kuhusu mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu.
Klipu ya video iliyohapo chini inmuonyesha Abdul Zahir akiseoma Surah moja ya Qur'ani kwa kuiga maqarii mbali mbali.
Abdul Zahir ana uwezo wa kuiga usomaji wa maqarii maarufu kama Sheikh Muhammad Ayub, Khalil al-Hisri, Mohamed al-Minshawi, Ali Abdullah Jaber, Fares Ibad na Mohamed Jibril.