IQNA

Ukosefu wa uadilifu, utumiaji mabavu ni dhati ya Mfumo wa Marekani

20:17 - June 03, 2020
Habari ID: 3472833
TEHRAN (IQNA)- Baraza la Mashauriano la Jumuiya za Kiislamu Malaysia limelaani vikali ukatili wa polisi nchini Marekani na kusema ukosefu wa uadilifu na utumiaji mabavu ni dhatu ya mfumo wa utawala nchini Marekani.

Katika taarifa baraza hilo limesema, maandamano ya sasa si malalamiko tu kuhusu kuuawa raia mweusi mikononi mwa afisa mzungu bali ni maandamani ya kupinga ubaguzi ulio katika mfumo wa Marekani ambao dhatu yake ni utumiaji mabavu na ukosefu wa uadilifu. Baraza hilo la Kiislamu Malaysia limelaani vikali mauaji ya Mmarekani mweusi au mwenye asili ya Afrika George Floyd, ambaye aliuawa kinyama na afisa mzungu. Aidha taarifa hiyo imesema kufuatia yanayojiri sasa Marekani, nchi hiyo haina haki tena ya kuzishinikiza nchi zingine kuhusu haki za binadamu.

Wakati huo huo, wananchi wenye hasira Marekani wameendeleza maandamano kwa usiku wa sita mfululizo kulaani mauaji ya Mmarekani mweusi aliyeuawa kinyama mikononi mwa polisi mzungu wiki iliyopita.

Aidha idadi kubwa ya wanajeshi na askari wa Gadi ya Taifa wametumwa katika miji mbali mbali kukabiliana na waandamanaji. 
Jumatatu ya wiki iliyopita, afisa mmoja mzungu wa jeshi la polisi la Marekani, anayejulikana kwa jina la Derek Chauvin, alimuua kikatili na kwa damu baridi kabisa, George Floyd Mmarekani mwenye asili ya Afrika katika mji wa Minneapolis huku wenzake watatu wakitizama na kuwazuia wapita njia wasimuokoe Mmarekani huyo. Ukatili huo umezusha wimbi kubwa la maandamano na machafuko katika kona zote za Marekani na sasa Rais Donald Trump ametangaza serikali ya kijeshi.

3471593

captcha