IQNA

Ubunifu wa Msikiti Saudia kwa wale wanaotaka kusoma Qur'ani Tukufu +Video

13:53 - June 22, 2020
Habari ID: 3472888
TEHRAN (IQNA) – Msikiti mmoja nchini Saudi Arabia katika eneo la Dammam umebuni nakala ya Qur'ani ya kidijitali kwa wanaoingia katika msikiti huo.

Kwa mujibu wa taarifa, msikito huo umebuni bakodi ambayo inawawezesha wanaofika hapo kuswali kuichukua taswira yake kwa kutumia simu za mkononi na hapo wanaweza kupata nakala ya Qur'ani.

Nakala hiyo ya Qur'ani ya kidijitali ina lugha mbali mbali na pia ina qiraa kwa sauti za wasomaji mashuhuri duniani.

Hatua hii imechukuliwa baada ya wataalamu wa afya kushauri kuwa waumini kwa sasa wasitumie misahafu iliyo misikitini kutokana na hofu ya kuambukizana ugonjwa wa COVID-19. Misikiti inawashauri waumini wasome Qur'ani kwa kutumia vifaa binafsi vya kielektroniki kama vile simu za mkononi au tableti.

3906210

captcha