IQNA

Mtaalamu wa UN aikosoa Israel kwa kuwaadhibu kwa umati Wapalestina

20:00 - July 18, 2020
Habari ID: 3472974
TEHRAN (IQNA)- Ripota na mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kuuzingira Ukanda wa Ghaza kunakofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuwaadhibu kwa umati wananchi wa Palestina.

Michael Lynk akisema hayo katika taarifa yake ya jana Ijumaa na kuongeza kuwa, mkakati wa Israel wa kuidhibiti jamii ya Wapalestina  ni uvunjaji wa haki za wananchi wa Palestina na ni kukanyaga misingi yote ya kisheria.

Ripoti huyo wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Kizayuni uache mara moja kuwatesa kwa umati wananchi wa Palestina ambapo kila siku watu milioni moja wasio na hatia wanapata matatizo. Amesema, kuuzingira Ukanda wa Ghaza kunachochea tu machafuko na migogoro mikubwa zaidi.

Vile vile amekosoa jinai za Israel za kuvunja nyumba za Wapalestina na kusema, tangu mwaka 1967 utawala wa Kizayuni wa Israel umeshavunja maelfu ya nyumba za Wapalestina kwa ajili ya kuwaadhibu.

Aidha ameonya kwamba jinai za Israel za kuendelea kuvunja nyumba za Wapalestina zinazidisha chuki tu na moto wa kulipiza kisasi katika nyoyo za Wapalestina.

Ripota huyo wa Umoja wa Mataifa pia amesema, jinai za Israel za kuwashambulia raia na kuwaua kidhulma Wapalestina katika vita kama vya siku 22 kwa kutumia kila aina ya silaha za kivita ni matukio ya kutisha ambayo yanamshitua na kumuhuzunisha mno kila mtu.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unauzingira Ukanda wa Ghaza tangu mwaka 2006. Kosa pekee lililofanywa na Wapalestina kwa mtazamo wa Israel, ni kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuichagua harakati ya HAMAS kuwaongoza.

3472027

captcha